Waziri mkuu wa Japan Shinzo Abe avalia kama Super Mario

Waziri mkuu wa Japan Shinzo Abe Haki miliki ya picha AFP
Image caption Waziri mkuu wa Japan Shinzo Abe

Sherehe za kufunga rasmi mashindano ya Michezo ya Olimpiki ya mwaka huu wa 2016, huko Rio De Jeneiro, nchini Brazil, zimemalizika usiku wa kuamkia leo.

Sherehe hizo sawa na zile za ufunguzi, zimefanyika katika uwanja wa Maracana, ambapo utengano wa kila timu ulivunjwa rasmi, baada ya washiriki wa Olimpiki kwa pamoja waliingia na kucheza uwanjani.

Hata hivyo, Wanariadha na watazamaji walioneka wakiwa wamechoka.

Haki miliki ya picha Ronald Grant
Image caption Waziri mkuu wa Japan Shinzo Abe

Lakini waziri mkuu wa Japan Shinzo Abe alipojitokeza akiwa amevalia mavazi yalio fanana yale ya muigizaji wa mchezo wa video Super Mario unaopatikana kwenye mchezo wa Nintendo watazamaji walianza kuchangamka upya.

Mchezo huo wa video wa Nintendo, hujulikana sana kwa mauzo ya nje kwa nchi hiyo ya Japan.

Hapo ndipo ulimwengu mzima ukapata taswira kamili ya michezo ya olimpiki itakayofanyika huko Tokyo mwaka 2020.

Haki miliki ya picha YOSHIKAZU TSUNO
Image caption Super Mario

Kwenye video ya Toyko2020, ilimuonyesha Mario akikimbia akiwa amefurahia huko Tokyo na akiruka katika bomba lenye rangi ya kijani kibichi ambalo muigizaji huyo hupenda kuingia kwenye mchezo huo wa video.