Nicolas Sarkozy, atangaza kuwania tena urais nchini Ufaransa

Nicolas Sarkozy Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Nicolas Sarkozy alishindwa na rais wa sasa Francoir Hollande miaka minne iliyopita

Rais wa zamani wa Ufaransa , Nicolas Sarkozy, amethibitisha kuwa atawania tena kiti hicho. Bw Sarkozy alishindwa na rais wa sasa Francois Hollande miaka minne iliyopita.

Wakati huo alisema kuwa anastaafu katika ulingo wa siasa, lakini katika kipindi cha miaka miwili alirejea katika harakati za kampeni.

Bw Sarkozy ni mmoja kati ya watu kadhaa wanaowania uteuzi wa kugombea urais kupitia chama cha mrengo wa kati na kulia akiwemo waziri mkuu wa zamani Francois Fillon, na waziri wa mambo ya kigeni Alain Juppe.

Bw Sarkozy anakabiliwa na kesi ya ufisadi na kujaribu kutoa rushwa katika uteuzi wa hakimu wa mahakama kuu ili atowe taarifa kuhusu uchunguzi kuhusiana na udhamini wa kisiasa.