Tetemeko kubwa latokea nchini Italia katika mji wa Umbria

Nguvu ya tetemeko hilo ni rishta 6.2
Image caption Nguvu ya tetemeko hilo ni rishta 6.2

Pametokea tetemeko kubwa katikati mwa Italia katika mji wa Umbria.

Watafiti wa Marekani wamesema kitovu cha tetemeko hilo kilikuwa katika mji wa Norcia, karibu na Perugia.

Nguvu ya tetemeko hilo ni rishta 6.2 na lilikuwa mbali kidogo na Mji wa Roma na Venice.

Wahudumu wa zima moto wamesema wamepokea taarifa za uharibifu wa baadhi ya majengo,huku kukiwa na taarifa chache juu ya tukio hilo.

Waziri mkuu wa Italia, Matteo Renzi, amesema serikali yake inaendelea kuwasiliana na taasisi za kiraia la ulinzi wa nchi hiyo.