Kenya kuanza kuuza mafuta 2017

Bomba la mafuta Haki miliki ya picha AFP
Image caption Bomba la mafuta

Kenya imetangaza kwamba itaanza kuzalisha na kuuza mafuta yake nje ya nchi kwa mara ya kwanza kuanzia mwezi Juni mwaka ujao.

Mwanzoni, Kenya inatarajia kuwa ikizalisha mapipa 2,000, lakini Rais wa taifa hilo Uhuru Kenyatta amesema nchi yake inatarajia kuwa muuzaji mkubwa wa mafuta katika kipindi cha miaka miwili itakayofuata.

Kenya iligundua mafuta miaka minne iliyopita eneo la Lokichar kaskazini magharibi mwa Kenya.

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Bomba la mafuta

Mafuta hao yatasafirishwa kwa barabara hadi bandari ya Mombasa kabla ya bomba la kusafirisha mafuta kutoka Lokichar hadi bandari inayojengwa Lamu kukamilika.

Ujenzi wa bomba hilo la urefu wa kilomita 850 unatarajiwa kukamilishwa kufikia mwaka 2021 .

Mapema mwaka huu, Uganda ilitangaza itajenga bomba lake la mafuta ambalo litapitia Tanzania badala ya kenya.