Polisi Ufaransa walazimisha mwanamke kuvua Burkini

Haki miliki ya picha VANTAGENEWS
Image caption Watalii katika ufuo wa bahari kusini mwa mji wa Nice

Picha zimeibuka zinazoonyesha polisi wa Ufaransa wakimlazimisha mwanamke wa Kiislamu kuvua vazi la kuogelea linalofunika mwili mzima linalojulikana kama Burkini katika ufuo wa bahari kusini mwa mji wa Nice.

Picha hizo zimezua mjadala mkali kuhusu kupigwa marufuku kwa vazi hilo la kuogelea na kubarizi.

Kisa hicho, kilifanyika ufukweni mahala ambapo zaidi ya watu wanane waliuawa katika shambulio lilifanywa na mtu mmoja mwenye itikadi kali hapo mwezi uliyopita.

Kundi la wakereketwa wa Kiislamu nchini Ufaransa wamesema wanawake 16 wametozwa faini katika kipindi cha wiki mbili zilizopita baada ya sheria mpya kupitishwa.

Haki miliki ya picha AP
Image caption Bahari iliyoko kusini mwa Nice

Lakini kundi hilo limesema miongoni mwa wanawake hao hakuna aliyekuwa amevalia vazi hilo.

Hii ni baada ya Ufaransa kupiga marufuku vazi hilo katika ufukwe.

Marufuku dhidi ya vazi la Burkini iliidhinishwa na mahakama ya mtaa husika lakini kesi hiyo itawasilishwa mbele ya mahakama ya utawala wa Ufaransa siku ya Alhamisi.