Tetemeko jingine la ardhi laikumba nchi ya Myanmar

Watu watatu wameripotiwa kufariki
Image caption Watu watatu wameripotiwa kufariki

Tetemeko jingine la ardhi lenye ukubwa wa rishta 6.8 limekumba mkoa wa kati wa Myanmar.

Watu watatu wameripotiwa kufariki katika tetemeko hilo ambalo lilisikika mpaka mji wa Bangkok nchini Thailand na Dhaka nchini Bangladesh.

Ndugu wawili wamekufa kwenye maporomoko.

Image caption Limesikika pia mji wa Bangkok nchini Thailand na Dhaka nchini Bangladesh

zaidi ya watu elfu moja waliokua wanasheherekea sherehe za kibudha wameathiriwa na tetemeko hilo.

Sehemu nyingine hazijaathiriwa sana.