Mwanamke alipia kukatwa viungo vyake kwa ajili ya malipo ya bima Vietnam

bara bara ya leri Hanoi
Image caption Awali alidai aligonjwa na treni kwenye njia ya leri ya Hanoi

Mwanamke mmoja nchini Vietnam amekiri kutoa mguu na sehemu ya mkono wake vikatwe ili aweze kudai malilipo ya bima, kulingana na polisi.

Mwezi Mei, mwanamke huyo mwenye umri wa miaka 30 , anayetambuliwa kama ''Ly Thi N", alidanganya kuwa aligongwa na treni, limeripoti gazeti la polisi nchini Vietnam.

Lakini kwa sasa ameripotiwa kukiri kwamba alimlipa rafiki yake dola $2,200 akate viungo vyake.

Lengo lilikua ni kudai dola zaidi ya $150,000 kutoka kwa kampuni ya bima yake.

Mtu aliyejifanya kuwa mpita njia aliyemuokoa kwa jina , "Doan Van D", ambaye ndiye aliyemkata viungo, aliita gari la kubebea wagonjwa/ambilance baada ya ''kumpata'' mwanamke aliyeumia katika bara bara ya Hanoi.

Picha zilizochapishwa na gazeti rasmi la polisi zilionyesha mwanamke huyo miezi mitatu baadae, akiwa amepona majeraha yake.

Anaaminiwa kuendesha biashara kwa shida, kwa mujibu wa vyombo vya habari nchini humo.

Tukio hili lisilo la kawaida limeibua mjadala mkali kwenye kwenye mitandao ya kijamii nchini Vietnam, huku wengi wakilaani kitendo hicho walichokitaja kama ufisadi mkubwa.