Watu weusi ni 'adui',asema Gavana wa Marekani

Gavana wa jimbo la Maine Paul LePage
Image caption Gavana wa jimbo la Maine Paul LePage

Gavana wa jimbo la Maine nchini Marekani amesema kuwa watu wa rangi ni 'adui' wa jimbo lake na kuonekana akipendekeza wapigwe risasi.

Akizungumzia kuhusu juhudi za jimbo la Maine kukabiliana na uhalifu wa dawa za kulevya,Paul LePage amesema kuwa adui mkubwa kwa sasa ni watu wenye rangi ama wale wa Hispanic.

''Wakati unapokwenda vitani,na adui anavaa nguo nyekundu na wewe unavaa nguo za rangi buluu ,unapiga risasi waliovaa nyekundu''.

Wanachama wakuu wa chama cha Democrat wamemtaka kujiuzulu.

Bwan LePage alitoa matamshi hayo alipokuwa akitaka kusahihisha matamshi aliyotoa hapo mbeleni yaliokosolewa kuwa ya kibaguzi.

Mada zinazohusiana