John Kerry akwama kwenye foleni Delhi, India

Wageni mashuhuri wanapozuru mji wa Delhi, hutarajia kupata barabara zikiwa wazi namna hii.

Haki miliki ya picha Getty Images

Lakini kwa raia wa kawaida, barabara huwa hivi...

Haki miliki ya picha Getty Images

... na hali huwa mbaya zaidi wakati wa mvua ya upepo wa msimu.

Haki miliki ya picha Getty Images

Lakini Waziri wa mambo ya nje wa Marekani John Kerry alipofika Delhi kwa mashauriano na maafisa wa serikali Jumatatu jioni, hakuwa na bahati.

Mvua kubwa ilinyesha na 'kukosa kutambua cheo chake'.

Badala ya magari yake kupitia barabara zilizo wazi, msafara wake wa magari ulikwama kwenye foleni zaidi ya saa moja.

Lilikuwa jambo lisilo la kawaida kwa sababu maafisa wa usalama huondoa magari barabarani kutengeneza njia ya kutumiwa na wageni mashuhuri.

Haki miliki ya picha NewsX

Watu kwenye mitandao ya kijamii walianza kufanyia mzaha masaibu hayo ya Bw Kerry. Baadhi, kama Karthik hapa alipendekeza Bw Kerry afanye wafanyavyo wenyeji mvua ikinyesha.

Haki miliki ya picha Karthik
Haki miliki ya picha Rajesh Mahapatra
Image caption Bw Mahapatra alipendekeza serikali serikali inunue helikopta za kuwasafirisha wageni mashuhuri