Wapenzi wa jinsia moja kuchangia damu Ireland Kaskazini

Pakiti ya damu
Image caption Pakiti ya damu

Marufuku iliowekewa wapenzi wa jinsia moja kutoa damu Ireland Kaskazini inatarajiwa kuondolewa siku ya Alhamisi.

Hatua hiyo inamaanisha kwamba wanaume ambao walifanya mapenzi na wanaume wenzao katika kipindi cha miezi 12 iliopita watakuwa huru kutoa damu iwapo wataafikia vigezo vya kutoa damu vinavyohitajika.

Mabadiliko hayo ya sera yalitangazwa na waziri wa afya Michelle O'neill mnamo mwezi Juni.

Mpango huo sasa unaileta pamoja Ireland Kaskazini na mataifa kama vile Uingereza,Uskochi na Wales.

Hatua hiyo inamaanisha kwamba wapenzi wa jinsia moja wanaweza kutoa damu iwapo watakuwa walifanya mapenzi katika kipindi cha miezi kumi na mbili iliopita.