Uturuki yatangaza kifo cha rais wa Uzbekistan

Rais wa Uzbekistan Islam Karomov
Image caption Rais wa Uzbekistan Islam Karomov

Rais wa Uzbekistan Islam Karimov amefariki,kulingana na Uturuki licha ya kutokuwa na habari rasmi kutoka kwa serikali yake.

Bwana Karimov mwenye umri wa miaka 78 alipelekwa hospitalini wiki iliopita baada ya kuvuja damu katika ubongo.

Hatahivyo serikali ya Uzbekistan imesema kuwa bwana Karimov ni mgonjwa sana.

Siku ya Ijumaa,waziri mkuu wa Uturuki Binali Yildrim aliambia mkutano uliopeperushwa hewani moja kwa moja kwamba rais Karimov alifariki.

Bwana Karimov alitawala Uzbekistan kiimla tangu mwaka 1989.

Hana mrithi wa moja kwa moja.Hakuna upinzani rasmi nchini humo na vyombo vya habari vinadhibitiwa na serikali.