Ajali yasababisha vifo vya watu 35 Afghanistan

Ajali yauwa watu 35 nchini Afghanistan
Image caption Ajali yauwa watu 35 nchini Afghanistan

Takriban watu 35 wamefariki na zaidi ya 20 kujeruhiwa mapema Jumapili, baada ya basi moja la abiria kugongana ana kwa ana na lori moja la kubeba mafuta, kusini mwa jimbo la Zabul, nchini Afghanistan.

Hayo ni kwa mjibu wa maafisa wakuu katika jimbo hilo.

Gavana wa jimbo hilo Bismillah Afghanmal, amesema kuwa basi hilo lilikuwa njiani kuelekea Kabul kutoka Kandahar, lilipogongana na tangi hilo la mafuta na kushika moto. Baadhi ya watu walichomeka kiasi cha kutotambuliwa.

Polisi wamesema baadhi ya majeruhi wamepelekwa katika hospitali kadhaa katika makao makuu ya jimbo la Qalat, na pia katika jimbo jirani la Kandahar.