Lil Wayne 'atangaza kustaafu' muziki

Lil Wayne Haki miliki ya picha AP

Lil Wayne ametangaza kwamba amestaafu kutoka kwenye tasnia ya muziki.

Aliandika kwenye Twitter: "Sasa sijiwezi tena, haka kiakili, na naondoka kwa staha na nashukuru mashabiki wangu."

Hata hivyo, hajafafanua iwapo ataacha sekta ya uimbaji kabisa, au ataacha tu uimbaji wa muziki wa kufoka.

Mwanamuziki huyo wa umri wa miaka 33 hata hivyo amesema hataki "kuonewa huruma".

Lil Wayne amekuwa akigonga vichwa vya habari hivi karibuni kwa visa mbalimbali.

Amekuwa an mzozo wa muda mrefu na Cash Money Records kuhusu kucheleweshwa kwa albamu yake ya 11, ambayo imepewa jina Tha Carter V.

Haki miliki ya picha AP

Alishutumu kampuni hiyo siku mbili zilizopita akitumbuiza na Drake mjini Miami.

Polisi Miami walifika nyumbani kwake kisiwa cha La Gorce baada ya mtu kupiga simu 911 akisema kulikuwa na ufyatuaji risasi. Habari hizo hazikuwa za kweli.

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii