Ayatollah Khamenei aishtumu Saudia inavyosimamia Hajj

Kiongozi wa kidini nchini Iran Ayatollah Khamenei
Image caption Kiongozi wa kidini nchini Iran Ayatollah Khamenei

Kiongozi mkuu wa kidini nchini Iran Ayatollah Ali Khamenei,ameishtumu Saudi Arabia jinsi inavyosimamia ibada za Hija za kila mwaka.

Kiongozi huyo amesema umma wa kiislamu sharti utafakari jinsi ibada hizo zinavyotekelezwa.

Mwaka jana kulishuhudiwa mkanyagano mbaya wa watu ambapo mahujaji wengi walipoteza maisha yao wakiwemo mamia ya raia wa Iran.

Mahujaji wa Iran hawataweza kushiriki ibada hiyo baada ya mazungumzo baina ya mataifa hayo mawaili yanayotofautiana juu ya mzozo katika mashariki ya kati kutibuka.