Watoto wachanga wanaovuma kwa uimbaji Kenya
Huwezi kusikiliza tena

Watoto wadogo wanaovuma kwa uimbaji Kenya

Kufanikiwa na kuwa mwanamuziki nyota nchini Kenya ni jambo ambalo huwa ngumu sana. Ala za muziki huwa ghali, maeneo ya kufanyia mazoezi hayapatikana na si wengi watakupa fursa kuonyesha kipaji chake.

Hata hivyo, watoto wawili Chris, 5, na Esther, 9, kutoka mtaa wa Mathare North tayari wamejijengea msingi kutokana na kipaji chao, na wanafanikiwa.

Wanafanya haya yote wakiendelea na masomo, na pia kutafuta wakati wa kucheza.