Dhuluma za kingono zakiandama kituo cha Fox,Marekani

Fox News Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Roger Ailes

Kituo cha habari cha Fox cha nchini Marekani kimetuliza malalamiko ya unyanyasaji wa kijinsia dhidi ya katibu mkuu wake Roger Ailes. Aliyechaguliwa waziwazi na Rupert Murdoch kuanzisha kituo cha habari cha kihafidhina na kuwa na mafanikio makubwa kwa kipindi cha takribani miaka ishirini.

Ailes alikanusha madai ya mmoja wa watangazaji maarufu wa mtandao wa cable, Gretchen Carlson, kwamba alitaka kufanya nae ngono. Lakini baada ya kukataa alimshushwa cheo na baadaye kumfukuzwa kazi.

Wanawake wengine zaidi wanalalamika kwa kutendewa vitendo sawa na hivyo. Bi Carlson anaonekana kukubali kuchukua dola milioni Ishirini kutoka kwa Fox, ambapo ilitaarifiwa kwamba zilitumika kuchunguza madai ya kuwatuliza wanawake wengine.