Volkswagen kuanza kutengeneza magari yake Kenya

Volkswagen
Image caption Volkswagen

Kenya imetia saini makubaliano na kampuni ya Volkswagen ya Afrika Kusini ili kutengeza magari hayo katika taifa hilo la Afrika Mashariki ,kulingana na taarifa ya serikali.

Volkswagen imeingia katika mkataba huo kwa kutumia kampuni ya kutengeza magari nchini Kenya KVM mjini Thika kuunganisha sehemu za magari hayo ikianza na gari lake maarufu la Volkswagen Vivo.

Thika ni mji wa viwanda ,uliopo kaskazini mashariki mwa mji mkuu wa Kenya Nairobi,na serikali ya Kenya inamiliki hisa katika kampuni hiyo.

Gari la kwanza la Volkswagen Vivo linatarajiwa kuunganishw akatika kiwanda hicho kufikia mwezi Disemba.

Kampuni hiyo ya ujerumani ilikuwa ikifanaya operesheni zake Kenya katika miaka ya 60 hadi mawaka 1977 ,ikiunganisha Mabasi ya Volkswagen,mabasi madogo na matatu ya kombi iliokuwa maarufu sana wakati huo.

Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta aliunga mkono wazo hilo.