Waasi wa Angola wa Flec wamedai kuwauwa wanajeshi wa serikali

Ramani ya nchi ya Angola
Image caption Waasi sasa wameripoti kutekeleza mauaji ya watu zaidi ya 50 tangu kuibuka kwa mapigano mapya mnamo mwezi Agosti

Makundi ya waasi yanayohasimiana katika jimbo lenye utajiri wa mafuta la Cabinda wanasema kuwa wamewauwa wanajeshi 12 wa serikali , Limeripoti wshirika la habari la Reuters.

Makundi hayo maarufu kama Flec wanasema wamewateka wanajeshi hao katika jimbo la kaskazini la Buco-Zau , karibu na mpaka wa nchi jirani ya Congo-Brazzaville siku ya Jumapili, shirika hilo limesema.

Waasi sasa wameripoti kutekeleza mauaji ya watu zaidi ya 50 tangu kuibuka kwa mapigano mapya mnamo mwezi Agosti, na serikali haijatoa kauli yoyote kujibu, ilinasema shirika la Reuters

Flec - kwa namna moja au nyingine wamekuwa wakiendesha mapigano kwa kiwango cha chini tangu miaka ya 1960.

kwa mara ya kwanza walianza mapigano ya silaha dhidi ya utawala wa ukoloni wa Ureno.

baada ya Angola kupata uhuru wake mwaka 1975 na Cabinda kuingizwa ndani ya utawala wa Angola, waasi wa Flec waliendeleza mapigano dhidi ya seriikali ya Luanda.