Rais Buhari awataka Wanigeria wabadili tabia

Rais Mahammadu Buhari Haki miliki ya picha Reuters
Image caption ''Tuachane na mienendo isiyofaa. Mabadiliko yanaanza na mimi na kila mmoja wetu lazima tubadilishe vile tunavyofanya mambo kwa mtindo wa kizamani.'' Amesema Buhari

Katika hotuba yake ya uzinduzi wa kampeni hiyo Buhari amesema: Si jambo la kutatiza leo hii kusema kwamba ukweli, kufanya kazi kwa bidii, na umungu vimepewa nafasi katika nyanja zote za ukiukaji wa sheria na kizazi katika maisha yetu ya kitaifa."

Rais huyo wa Nigeria amewataka watu wa Nigeria kwa ujumla kubadili tabia.

Amesema: "tunapaswa kukubali mabadiliko ya mtazamo wa mabadiliko katika maisha yetu ya kibinafsi na ya umma pamoja''.

Haki miliki ya picha @FMICNigeria
Image caption Nembo ya kampeni ya rais wa Nigeria Mahammadu Buhari imetangazwa kwenye mtandao wa twitter

''Tuachane na mienendo isiyofaa. Mabadiliko yanaanza na mimi na kila mmoja wetu lazima tubadilishe vile tunavyofanya mambo kwa mtindo wa kizamani.'' Amesisitiza Bw Buhari.

Serikali inatumia #ChangeBegiunsWithMe (MabadilikoYanaanzaNaMini) kwenye mtandao wa Twitter kutangaza ujumbe wake, lakini inaonekana si raia wote wa Nigeria wanaounga mkono kampeni hii: Mfano Akintomide ‏@Tomyboiz ameandika: Tafadhali wanigeria lazima tuwe tayari kupinga wito huu wa #ChangeBeginsWithMe, ni upuuzi, mabadiliko lazima yaanze na serikali na wanasiasa.

Mwingine ameandika: ''Buhari utaleta mabadiliko pale utakapoacha kulaumu utawala uliopita na kuwajibika kikamilifu na utawala wako, huu ndio ushauri wangu''