Mashambulizi makali yasababisha vifo Syria

Mashambulizi makali nchini Syria Haki miliki ya picha AFP
Image caption Mashambulizi makali nchini Syria

Mashambulizi makali ya ndege katika anga ya Syria yamesababisha vifo vya makumi ya watu, siku moja tu baada ya Marekani na Urusi kutangaza kuwa vita katika nchi hiyo vitasitishwa mnamo Jumatatu.

Wakereketwa katika maeneo yaliyoshambuliwa wanasema kuwa watu 45 waliuawa katika makaazi yaliyoshambuliwa na katika vitongoji vyake.

Katika mji unaokaliwa na waasi wa Idlib, ripoti zinasema watu wengine 40 waliuawa, kukiwemo wengi waliokuwa wakinunua mboga na matunda.

Serikali ya Syria na kundi kuu la upinzani linaloshiriki katika mashauriano ya amani wameunga mkono mkataba huo ulioafikiwa mjini Geneva.

Iwapo mkataba huo wa amani utatekelezwa na utangamane kwa angalau juma moja, Marekani na Urusi zinatarajia kushirikiana katika mashambulizi dhidi ya washambuliaji wa Kiislamu wenye itikadi kali.