Platini kuhutubia bodi ya Uefa

Malipo yaliyosababishwa Platini atimuliwe bado yanafanyiwa uchunguzi Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Malipo yaliyosababishwa Platini atimuliwe bado yanafanyiwa uchunguzi

Michel Platini ameruhusiwa kuhutubia bodi ya shirikisho la Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya Uefa wakati watakapokutana wiki hii licha ya rais huyo wa zamani kupigwa marufuku ya kushiriki katika shughuli zote za kandanda.

Mfaransa huyo mwenye umri wa miaka 61, alikuwa kiongozi wa Uefa hadi pale alipopigwa marufuku ya ukiukaji wa sheria dhidi ya dola milioni 1.3, malipo yaliyo kinyume cha sheria'.

Uefa itakutana kumteua atakayemrithi Platini, mchezaji wa zamani wa timu ya taifa ya Ufaransa

Bodi hiyo iliomba idhini kwa Fifa kwa kiongozi wao wa zamani kushiriki katika mkutano huo.

'Kamati ya maadili ya Fifa imefahamisha Shirikisho la soka Uefa kwamba Michel Platin ataruhusiwa kushiriki katika kongamano la 12 lisilo la kawaida mjini Athens tarehe 14 mwezi Septemba , imesema katika tarifa yake.

"Ombi la bwana Platini kuhudhuria mkutano huo lilitolewa na Uefa na tumekaribisha uamuzi huo," taarifa hiyo imeongeza.