Beki wa Crystal Palace Souare atibiwa baada ya ajali

Pape Souare Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Pape Souare

Beki wa klabu ya Crystal Palace Pape Souare anaendelea na matibabu hospitalini baada ya kupata ajali ya gari hapo jana.

Souare mwenye umri wa miaka 26 aliumia mguu na taya hivyo ataendelea kupatiwa matibabu mpaka atapokuwa amepona .

Taarifa kutoka klabuni kwake inasema timu hiyo inashirikiana kwa ukaribu na Hospital pamoja na familia kuhakisha maendeleo ya mchezaji huyo yanakua mazuri.

Mchezaji huyu raia wa Senegal alisajiliwa na Crystal Palace mwaka 2015 akitokea, Klabu ya Lille ya Ufaransa na alicheza mchezo wa ligi wa msimu huu dhidi ya Bournemouth.