Shimon Peres akimbizwa hospitalini baada ya kuugua ghafla

Peres ameshika nyadhifa nyingi serikalini
Image caption Peres ameshika nyadhifa nyingi serikalini

Aliyekuwa Rais wa tisa wa Israel , Shimon Peres , amekimbizwa hospitali iliyopo nje kidogo ya mji mkuu wa Tel Aviv baada ya kuugua kiharusi.

Taarifa kutoka ofisi ya Perez inasema kuwa amekuwa akipumua kwa msaada wa kifaa maalum.

Mnamo mwezi Januari mwaka huu Perez alifanyiwa upasuaji mdogo wa moyo baada ya kuugua mshtuko wa moyo.

Image caption Peres alishinda tuzo ya amani ya Nobel 1994 kwa kuongoza mazungumzo ya amani na Palestina

Msindi huyo wa tuzo ya nobel ametimiza umri wa miaka 93 mwezi uliopita na amewahi kushikilia nyadhifa za juu zaidi katika serikali ya Israel.

Aliachia madaraka ya urais mwaka 2004.