Wanamazingira waandamana Nairobi kupinga ujenzi wa reli mbugani

Waandamanaji mjini Nairobi wakipinga ujenzi wa reli ya kisasa ndani ya mbuga ya wanyama ya Nairobi
Image caption Waandamanaji mjini Nairobi wakipinga ujenzi wa reli ya kisasa ndani ya mbuga ya wanyama ya Nairobi

Kundi la wahifadhi wa mazingira na wenyeji wa vijiji vilivyo karibu na mbuga ya wanyama ya Nairobi, wameandamana wakipinga mpango wa kutumia sehemu ya mbuga hiyo katika ujenzi wa reli ya kisasa (SGR)

Reli hiyo inayokadiriwa kugharimu dola bilioni tatu, ni mradi mkuu wa serikali ya Rais Uhuru Kenyatta, itakayounganisha mji wa Mombasa na Kisumu, umbali wa kilomita 482.

Shirika la kitaifa linalohudumia wanyama pori lilikubali serikali kujenga daraja inayopitia kwenye mbuga hiyo, ili kuhakikisha kwamba wanyama hawasumbuliwi na makelele.

Image caption Reli hiyo inayokadiriwa kugharimu dola bilioni tatu, ni mradi mkuu wa serikali ya Rais Uhuru Kenyatta, itakayounganisha mji wa Mombasa na Kisumu, umbali wa kilomita 482.

Waandamanaji hao wanasema hawakuhusishwa katika kufanya uamuzi huo.

Waandamanaji hao waliandamana hadi makao makuu ya Shirika la kitaifa linalohudumia wanyama pori, kuwasilisha ombi lao, na kutoa mapendekezo ya maeneo mbadala ambapo reli hiyo inaweza kujengwa.