Mwanamuziki Coolio akamatwa Marekani

Mwanamuziki Coolio Haki miliki ya picha AFP
Image caption Mwanamuziki Coolio

Mwanamuziki Coolio amekamatwa katika uwanja wa ndege wa Los Angeles baada ya bunduki iliojaa risasi kupatikana katika bagi moja alipofanyiwa ukaguzi ,kulingana na mamlaka nchini humo.

Coolio ni maarufu sana kwa wimbo wake Gangsta Paradise ambao ulitolewa mwaka 1995.

Maafisa wa polisi katika uwanja wa ndege wa Los Angeles walifahamishwa kuhusu ugunduzi huo uliofanywa na maafisa wa usalama katika uwanja huo.

Walimkamata mtu mmoja aliyesema kuwa begi hilo lilikuwa lake.

Uchunguzi ulibaini kwamba begi hilo lilikuwa na vitu vilivyokuwa vikimilikiwa na mtu mwengine ambaye alitambulika kuwa Coolio ambaye alikuwa akisafiri na mtu huyo.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Coolio

Mtu wa pili alikuwa tayari ashapita katika eneo la ukaguzi na kupanda ndege.

Maafisa wa polisi walimtambua mshukiwa wa pili ambaye jina lake ni Coolio na alikamatwa kwa tuhuma za kumiliki bunduki.

Coolio ni maarufu sana kwa wimbo wake Gangsta Paradise ambao ulitolewa mwaka 1995.