Uchaguzi hauwezi kufanyika mwaka huu DR Congo
Huwezi kusikiliza tena

Tume: Uchaguzi hauwezi kufanyika mwaka huu DR Congo

Tume ya Uchaguzi nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo imesisitiza kwamba haiwezekani kufanya uchaguzi nchini humo mwaka huu kama ilivyoelezwa kwenye katiba.

Mchakato wa kufanyika kwa uchaguzi ulitarajiwa kuanza leo lakini tume hiyo imesema hilo haliwezekani na badala yake inataka uchaguzi ufanyike mwaka ujao.

Makundi ya upinzani yamepanga maandamano leo kupinga kuandaliwa kwa kalenda mpya ya uchaguzi.

Mwandishi wa BBC Mbelechi Msochi anaarifu zaidi.