Juhudi za kuokoa jamii ya Yaaku
Huwezi kusikiliza tena

Juhudi za kuokoa jamii ya Yaaku, Kenya

Wa-Yaaku, ni moja ya makabila madogo kabisa yaliyo hatarini kutoweka duniani.

Wa-Yaaku wanaishi Kenya. Wamesalia wazee tisa tu wanaoweza kuzungumza lugha ya Kiyaaku kwa ufasaha.

Kwa mujibu wa Shirika la Umoja wa Mataifa UNESCO, kabila la wa-YAAKU lina watu elfu nne tu. Lugha yao iko hatarini kupotea iwapo hatua yoyote haitachukuliwa kuiihifadhi. UNESCO linasema zaidi ya nusu ya lugha zote zinazozungmzwa duniani ziko hatarini kutoweka.

Emmanuel Igunza amezungumza na wazee wa Ki-Yaaku.