Kijiji ambacho wanawake huwabeba wanaume
Huwezi kusikiliza tena

Kijiji ambacho wanawake 'huwabeba wanaume' Rwanda

Katika kisiwa Nkombo, kilichopo magharibi mwa Rwanda katika ziwa Kivu, kuna utamaduni wa kipekee usiokuwepo popote pale nchini Rwanda ambapo wanawake huwaosha miguu waume zao, kuwapaka mafuta na kuwabeba mgongoni hadi kitandanani.

Wanawake walioozungumza na BBC wanasema utamaduni huo sio kudhalilisha mwanamke wala mke kunyenyekea mmewe kupindukia bali ni kuonesha upendo.

Wanaume wanasifia sana utamaduni huo kiasi kwamba baada ya ndoa hutoa mahari tena mara nyingi iwezekanavyo.

Mwandishi wa BBC Yves Bucyana ametembelea kisiwa hicho na hii hapa ni taarifa yake.