Magufuli avunja bodi ya udhamini wa pensheni Tanzania

Magufuli Haki miliki ya picha Ikulu, Tanzania
Image caption Rais Magufuli pia amevunja bodi ya udhamini wa mfuko huo

Rais wa Tanzania John Magufuli ametengua uteuzi wa Mwenyekiti wa Bodi ya Udhamini ya Mfuko wa Pensheni wa LAPF Prof Hasa Mlawa na kuvunja bodi ya udhamini wa mfuko huo.

Taarifa kutoka ikulu imesema uamuzi huo utaanza kutekelezwa mara moja.

"Uteuzi wa Mwenyekiti mpya wa Bodi ya Udhamini ya LAPF utafanywa baadaye," taarifa hiyo imesema.