Kwa Picha: Hoteli ya kifahari inayoishi maskini Msumbiji

Grande Hotel katika mji wa Beira pwani ya Msumbiji inahifadhi maskwota 3,500. Mpiga picha Fellipe Abreu alitembelea mjengo huo ambao kwa wakati mmoja uliitwa "Fahari ya Afrika":

Haki miliki ya picha Fellipe Abreu
Image caption Watu kwenye ngazi ya Grande Hotel katika mji wa Beira pwani ya Msumbiji
Haki miliki ya picha Fellipe Abreu
Image caption Ilipofunguliwa 1955, ilikuwa nimojawapo ya hoteli za kifahari Afrika. Ni jengo lenye orofa 3…
Haki miliki ya picha Fellipe Abreu
Image caption ... Dimbiwi la kuogolea - sasa linatumika kufuwa nguo - ngazi ndefu,maduka, migahawa, ofisi ya posta, sinema, na vyumba 122.
Haki miliki ya picha Fellipe Abreu
Image caption Ilitarajiwa pia kuwa na sehemu ya kucheza kamari, lakini wamiliki walishindwa kupata kibali kutoka kwa maafisa wa kikoloni wa Ureno.
Haki miliki ya picha Fellipe Abreu
Image caption Hapa ndipo matatizo yalipoanza licha ya kuwa Beiran ni mji maarufu wa pwani ya bahari hindi, hoteli haikuweza kuvutia wageni wengi.
Haki miliki ya picha Fellipe Abreu
Image caption Ilifungwa 1963 na ilitumika kwa hafla na sherehe kubwa pekee.
Haki miliki ya picha Fellipe Abreu
Image caption Wakati wa vita vya kiraia mwishoni mwa miaka ya 70, ilikuwa kambi ya jeshi na gereza kwa wafungwa wa kisiasa.
Haki miliki ya picha Fellipe Abreu
Image caption Baada ya kufungwa kwa hoteli hiyo katika mwongo uliofuata iliporwa na watu wakaingia kuishi hususan waliokuwa wanatoroka vita.
Haki miliki ya picha Fellipe Abreu
Image caption Kwa mara ya kwanza, hoteli ilijaa watu. Kwa sasa imezidi kima chake cha kawaida wakati familia wanaishi katika kila sehemu ya hoteli hiyo yenye kiza, na joto jingi, ikiwemo wanaoishi kwenye ngazi.
Haki miliki ya picha Fellipe Abreu
Image caption Kumetengenezwa sehemu ya burudani ya kutizama filamu katika sehemu ya pekee ilo na umeme katika hoteli hiyo. kwa kawaida kuna watoo na watu wazima wanaokaa kutizama TV
Haki miliki ya picha Fellipe Abreu
Image caption Baadhi ya familia sasa wanaishi katika hoteli hiyo kwa vizazi vitatu. miaka 24 tangu kumalizika vita vya kirai , zaidi ya idadi nusu ya raia Msumbiji wanaendelea kuishi katika umaskini.
Haki miliki ya picha Fellipe Abreu
Image caption Kwasababu hoteli hiyo haitizamwi, jengo lina matatizo huku miti ikimea juu.
Haki miliki ya picha Fellipe Abreu
Image caption Usafi pia ni tatizo , taka za miaka kadhaa zimekusanyika na mgahawa mmoja unatumika kama choo siku hizi.
Haki miliki ya picha Fellipe Abreu
Image caption Mkaazi huyu anaikarabati hoteli hii, ana anatengeneza matofali ya kukarabati eneo lililo chomeka na moto.
Haki miliki ya picha Fellipe Abreu
Image caption Watu wanaoishi Grande Hotel hawalipi kodi , lakini kumewekwa sheria na hakuruhusiwi wakaazi wapya kwasababu wanasema hoteli imejaa.
Haki miliki ya picha Fellipe Abreu
Image caption Viongozi wa jamii katika eneo hilo, kama Carlos Nori (kwenye picha), wanachaguliwa na wakaazi na kuna baraza linalokutana kila mwezi kujadili matatizo yoyote.
Haki miliki ya picha Fellipe Abreu
Image caption Na pia wanapanga michezo. "karibu kila siku, wanaume hukutana nje na kucheza soka," anasema bwana Nori.

Kuhusu BBC