Wakimbizi walalamikia hali mbaya inayowakabili Daadab

Jubaland kwa sasa imekataa kupokea wakimbizi zaidi
Image caption Jubaland kwa sasa imekataa kupokea wakimbizi zaidi

Maelfu ya wakimbizi wa Somalia wamekwama katika kambi ya Dadaab Refugee kaskazini mashariki mwa Kenya baada ya jitihada za kuwarudisha nyumbani kusitishwa takriban mwezi mmoja uliopita.

Utawala wa Jubaland nchiniSomalia umekataa kupokea wakimbizi hao kufuatia mzozo na Shirika la Umoja wa mataifa linalowashughulikia wakimbizi UNCR na serikali ya Kenya.

Hivi sasa baadhi ya wakimbizi wameiambia BBC kwamba wameuza mali zao tayari kurudi nyumbani na sasa hawana mahali pa kwenda.

Hawa Mohamed Muse ni mmoja wa wakimbizi waliokwama. '' Hatuna chakula, kuna baridi usiku na hatuna mahali pa kujihifadhi.

Image caption Baadhi wanasema wanatumia nguo kujiking ana baridi

''Tunaishi chini ya miti, tunapata chanjo tu kwa watoto wetu lakini hakuna dawa kwa watu wazima. Hatuna mipango yoyote tunasubiri tu kauli ya Umoja wa mataifa", anasema Hawa.

Haya yanatokea wakati viongozi wa dunia wanakutana New York katika kikao maalum kuuhsu mzozo wa wakimbizi duniani.

Msemaji wa UNHCR ameiambia BBC kwamba wanawashughulikia wakimbizi 2000 waliopo katika kituo cha muda wakisubiri kuanza upya mpango wa kurudisha nyumbani. Amekana kuwa wakimbizi hao wapo katika hali mbaya.