Wasomi wa Ghana: Mahatma Gandhi ''alibagua watu weusi''

Mahatma Ghandi Haki miliki ya picha DANIEL OSEI TUFFUOR
Image caption Sanamu ya Mahatma Ghandi

Kiongozi mashuhuri Africa Nelson Mandela alisema mafundisho ya Mahatma Gandhi yalisaidia katika harakati za raia weusi wa Afrika kusini kuuangusha utawala wa kibaguzi wa makaburu weupe nchini humo.

Aliyekuwa mtawala nchini Ethiopia Haile Selassie I, alielezea jinsi alivyomuenzi akisema "Mahatma Gandhi daima atakumbukwa kwa miaka yote na hasa wale ambao wanapenda uhuru na haki duniani.

Lakini je kuna vijimambo vilivyojificha kuhusu misimamo ya kibaguzi aliyokuwa nayo Gandhi ambayo haikubainika waziwazi machoni pa watu?

Sasa imeibuka kwamba si wote Afrika wanampa hadhi ya juu Mahatma Gandhi ambae pia anajulikana kama 'Baba wa Taifa la India".

Waraka wa uchanganuzi wa swala hilo umeanzishwa kwenye mtandao na zaidi ya wahadhiri wa chuo kikuu cha Ghana na umeetiwa saini na zaidi ya watu 1,000 .

Wanataka sanamu ya Mohandas Karamchand Gandhi iondoshwe kutoka maeneo ya chuo hicho kikuu huko mjini Accra.

Wasomi hao wasema japo sera ya Gandhi,iliyokuja kujulikana vyema kama 'non-violent movement' yaani kupigania uhuru kutoka kwa utawala wa kikoloni wa muingereza pasi na kutumia njia za kivita hapo katikati ya karne ya 20, pia ilikuwa na ''doa la ubaguzi wa rangi".

Waraka huo umeorodhesha nukuu za kiongozi huyo wa zamani wa India, ambazo kwa wakati fulani aliwaita Waafrika''savages or the Natives of Africa'' yaani "nduli, wasio na ustaarabu " na wakati mwengine hata kutumia neno "kaffirs"

Mfano mmoja ni katika barua ambayo Gandhi alilindikia bunge la Afrika kusini hapo 1893 akisema "mtazamo ulioenea katika maeneo yaliyochini ya ukoloni ni kwamba wahindi ni watu bora kwa kiwango fulani kuliko hao nduli asilia wa Afrika."

Nukuu hizo zote zimetolewa kutoka tovuti ya utafiti Gandhi Serve, ambayo imekuwa ikihifadhi kazi na kumbukumbu za Mahatma Gandhi.

Kwa hivyo waraka wa wasomi hao wa Ghana unauliza ''Je wanahistoria wataeleza vipi kinaya hiki kwamba waafrika wanamtukuza Gandhi kwa kujenga sanamu lake maeneo ya chuo chetu kikuu huku kuna ushahidi bayana kwamba alikuwa akiwabeza Waafrika?"

Sanamu hilo ilikuwa zawadi iliyopewa serikali ya Ghana na rais wa India Pranab Mukherjee, hapo Juni.

Haki miliki ya picha Twitter
Image caption Hafla ya kuweka sanamu ya Ghandi iliyozua utata huko Ghana

Lilipowekwa lilikashfiwa papo hapo, baadhi wakitumia hashtags #GandhiMustComeDown.. yaani lazima sanamu la Ghandi lishukishwe chini.

Daniel Osei Tuffuor, mwanafunzi wa zamani wa chuo kikuu cha Ghana, akiweka saini yake kwenye waraka huo ameiambia BBC "WAGhana wawe na ujasiri wa kuwakuza mashujaa wetu halisi wake na wakiume. Hamkuwa na chochote cha amani katika sera ya Gandhi. Yeyote anaehubiri amani na utulivu na kisha kuendeleza itikadi za kibaguzi ni mnafiki! ."

Na inavyoelekea utata huo wa mtazamo wa Gandhi kwa waafrika si swala geni.

Aliyeaandika wasifa wake ambae pia ni mjukuu wake Rajmohan Gandhi, alisema babu yake alikwenda Africa kwa mara ya kwanza akiwa na umri wa miaka 24 kufanya kazi kama wakili .kwa hivyo 'Bila shaka hakuwa na uelewa mzuri na hivyo ''kimakosa aliwabeza raia weusi wa Afrika kusini''.

Haki miliki ya picha Hulton Archive
Image caption Ghandi alipokuwa wakili kijana akifanya kazi huko Afrika kusini( 1869 - 1948) enzi za ubaguzi wa rangi

Dr Obadele Kambon, mmoja wa walianzisha waraka huo wa malalamishi anasisitiza kuwa ni vyema kwenye nafasi hiyo ya sanamu ya Ghandi iwekwe ile ya kiongozi mwengine yeyote wa kiafrika awe wa kitamaduni au wa kisasa ambae ataendeleza na kuwakilisha maadili mema ya mwafrika kujitambua na kujiheshimu

Ameongeza kusema " Kwa lengo la mda mrefu tungependa kuungana na harakati za wote duniani wanaoendeleza sera za kujivunia uasili wa mtu na ustaarabu wake hivyo tungependa kuona kufanikiwa kwa kampeni kama zile za kuondosha sanamu la Rhodes huko Umzantsi (Afrika Kusini), maandamano ya Colin Kaepernick dhidi ya mwimbo na bendera ya kibaguzi ya Marekani na vilevile kufanikiwa kwa maandamano ya kujali maisha ya mtu mweuzi iliyobadikwa jina 'the Black Lives Matter protests''.

"Mwisho wa yote taswira yetu waafrika ikue kwa manfaa ya saikolojia ya Mwafrika na wala si sanamu za wale waliotuita ''nduli'' ... Sanamu ya Gandhi ianguke Africa iiinuke!"

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii