FBI huenda likamchunguza Brad Pitt

Brad Pitt
Image caption Brad Pitt

Shirika la ujasusi nchini Marekani FBI linakusanya habari kuhusu kisa kimoja kunachomuhusisha nyota wa filamu Brad Pitt na wanawe walipokuwa wameabiri ndege ya kibinafsi wiki iliopita.

Shirika hilo linaangazia uwezekano wa kuanzisha uchunguzi au la.

Mkewe Pitt ,Angelina Jolie anataka kumpatia talaka muwewe kutokana na kile alichokitaja kuwa tofauti zisizotatulika.

Jolie ametaka apewe watoto wote sita huku akimtaka jaji ampatie haki za kuwatembelea watoto hao mumewe.

Shirika hilo la ujajusi liliambia BBC: Kutokana na ombi lenu kufuatia madai yaliotolewa kuhusu ndege iliokuwa ikimbeba bwana Pitt na wanawe ,FBI linaendelea kukusanya ukweli na litaamua iwapo litaanza uchunguzi au la.

Pitt alitoa taarifa katika gazeti la People baada ya Jolie kuwasilisha ombi la kutaka talaka,akisema ameshtushwa na hatua hiyo na kuongezea: kitu muhimu ni maisha mazuri ya watoto wetu.

''Ninaviomba vyombo vya habari kutowahangaisha wakati huu mgumu''.