Mhadhiri ashtakiwa 'kwa kumtusi rais Magufuli kwa WhatsApp'

Sheria ya uhalifu wa mtandao Tanzania
Image caption Sheria ya uhalifu wa mtandao Tanzania

Muhadhiri mmoja mkuu ameshtakiwa katika mahakama moja nchini Tanzania kwa kumtusi rais wa taifa hilo chini ya sheria ya uhalifu iliowekwa mwaka uliopita.

Kulingana na afisi mkuu wa polisi wa eneo la kusini magharibi mwa Tanzania, shtaka hilo ni hatia na mtu anaweza kufungwa hadi miaka mitatu jela ama kupigwa faini ya dola 3,000 ama zote.

Mhadhiri huyo amekana mashtaka hayo.

Mhadhiri huyo ni mtu wa kumi kushtakiwa chini ya sheria hiyo.

Wale ambao wameshtakiwa kwa kumtusi rais Magufuli katika miezi ya hivi karibuni ni pamoja na viongozi wa upinzani.

Mnamo mwezi Machi,shirika la kukabiliana na changamoto za milenia nchini Marekani chini ya USAID, lilifutilia mbali ufadhili wa dola milioni 500 kwa taifa la Tanzania kufuatia wasiwasi wa kuidhinishwa kwa sheria hiyo ya uhalifu wa mitandaoni.