Vilabu vya Israel vyatakiwa kuondoka West Bank

Eneo la West Bank linalokaliwa kimabavu na Israel
Image caption Eneo la West Bank linalokaliwa kimabavu na Israel

Shirika la kutetea haki za kibinadamu Human Rights Watch limelitaka shirikisho la soka duniani Fifa kuziamuru timu 6 za vilabu vya soka vya Israeli kuondoka kutoka eneo linalokaliwa na walowezi huko West Bank wakisema maeneo hayo yanakaliwa kimabavu kinyume na sheria za kimaaifa.

Human Rights Watch imesema kuruhusu timu hizo kuendelea na shughuli zake za kucheza soka katika ardhi ya Palestina FIFA inavunja sheria zake yenyewe.

Huku FIFA ikiwa inatarajiwa kulijadili swala hilo katika kikao chake cha Octoba, utawala wa Israeli unasema FIFA haina mamlaka ya kuiamuru Israel kuhusu swala hilo.