Jordan:Waziri mkuu alaumiwa kwa mauaji ya mwandishi wa vitabu

Hattar alishambuliwa sana katika mitandao ya kijamii baada ya kuweka kibonzo hicho
Image caption Hattar alishambuliwa sana katika mitandao ya kijamii baada ya kuweka kibonzo hicho

Mtoto wa mwandishi wa vitabu nchini Jordan ambaye alipigwa risasi na kuuwawa siku ya Jumapili amemtuhumu waziri mkuu wa nchi hiyo kuwa ndiye anayewajibika na anapaswa kujiuzulu.

Akiongea na BBC, Mutasem Hattar alisema kuwa familia yake haitamzika baba yake ,Nahed, mpaka pale Mfalme Abdallah atakapo mlazimisha waziri mkuu Hani al-Mulki kujiuzulu.

Anasema kwamba Bwana Mulki alichochea uadui ambao ulipelekea mauaji ya baba yake wakati akiingia mahakamani akishtakiwa kwa kosa kusambaza kibonzo kinachodaiwa kuwakasirisha baadhi ya waisilam.

Mutasem Hattar anasema ilikuwa ni jambo la wazi kwamba kibonzo hicho kilikuwa kinahusu kundi la kigaidi la IS- na alimsifu baba yake kwa kujitoa sadaka kwa ulimwengu.