Ali Bongo aapishwa kwa muhula wa pili

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Bongo alishinda kwa kura zisizozidi 6000

Rais wa Gabon Ali Bongo ameapishwa kwa muhula wa pili wa miaka saba kufuatia uchaguzi uliokumbwa na utata ambapo watu kadhaa waliuawa.

Kuapishwa huku kunafanyika siku tatu baada ya mahakama ya katiba kukataa shinikizo za upinzani za kutaka kura kuhesabiwa tena.

Ali Bongo ambaye babake Omar Bongo alikuwa rais wa Gaboin kwa miongo minne, alishinda uchaguzi huo kwa kura zisizozidi 6000.