Afya ya Shimon Perez wa Israel yazorota

Israel Haki miliki ya picha Google
Image caption Shimon Perez

Taarifa kutoka nchini Israel zinaeleza kuwa afya ya mwanasiasa mkongwe na waziri Shimon Peres imezorota mno .Ndugu wa karibu wakiongozi huyo wa zamani ndiyo wenye ruhusa ya kwenda katika hospitalia aliyolazwa yapata wiki mbili zilizopita kutokana na tatizo la kushambuliwa na kiharusi mara kadhaa.

Ikumbukwe kwamba Shimon Peres ameitumikia nchi hiyo kama waziri mkuu mara mbili na mara moja katika nafasi ya Rais.Simon pia aliwahi kutunukiwa tuzo ya amani ya Nobel kwa ushiriki wake mkubwa katika harakati za kutafuta suluhu ya mgogoro wa kisiasa baina ya Israel na Palestina mnamo miaka ya 1990.

Shimon Perez ni miongoni mwa kizazi cha mwisho cha wanasiasa walioshuhudia kuzaliwa kwa taifa jipya la Israel mnamo mwaka 1948 .