Ghasia zashuhudiwa nchini Ethiopia

Waandamanaji wakabiliana na maafisa wa polisi Ethiopia
Image caption Waandamanaji wakabiliana na maafisa wa polisi Ethiopia

Ripoti kutoka nchini Ethiopia zinasema kwa kumeshuhudiwa ghasia kati ya vikosi vya usalama na waandamanaji wanoipinga serikali.

Shirika la habari la Reuters liliwanukuu walioshuhudia wakisema kuwa polisi walifyatua risasi na gesi ya kutoa machozi katika mji wa Bishoftu ulio eneo la Oromiya.

Eneo hilo pomoja na lile lililo karibu la Amhara yamekumbwa na ghasia mbaya ambapo mamia ya watu wameuawa wakati jamii zinapinga kile zinataja kuwa dhuluma za serikali.