Vikosi vya majini vyaokoa maelfu Italia

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Vikosi vya majini na wahamiaji barani ulaya

Vikosi vya majini nchini Italia vimesema zaidi ya wahamiaji elfu sita waliokuwa wakijaribu kuingia barani ulaya wameokolewa maji hapo jana.

Idadi hiyo imesemekana kuwa kubwa sana kwa siku moja.

Wahamiaji hao waliokuwa wakitokea nchini Libya walikuwa wamesheheni katika boti walizokua wanaitumia.

Maiti tisini zimeweza kupatikana na miongoni mwa maiti hizo ni ya mwanamke mjamzito mwenye umri wa miaka ishirini na tatu.

Vikosi hivyo vinavyoshika doria katika fukwe ya bahari ya Mediterania nchini Italy wamesema zaidi ya watu mia saba walikuwa wamepanda katika boti hiyo na watoto wapatao mia mbili.