Moise Katumbi apanga kurejea DRC
Huwezi kusikiliza tena

Moise Katumbi asema anapanga kurejea DRC

Uchaguzi katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo utacheleweshwa hadi mwaka 2018 kwa mujibu wa tume ya uchaguzi.

Rais Joseph Kabila amekuwa madarakani kwa miaka 15 lakini katiba haimruhusu kuwania urais kwa muhula wa tatu.

Vyama vya upinzani vimekuwa vikimlaumu Rais Kabila, kwa makusudi kuchelewesha uchaguzi, ili aendelee kuwa madarakani hata wakati muhula wake utakapomalizika, mwezi Desemba.

Salim Kikeke alizungumza na kiongozi wa chama kimoja cha Upinzani katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo Moise Katumbi na kumuuliza kama atarudi nyumbani Congo.