Haiti yapigwa na kimbunga Matthew

Jamaica pia imeathirika na kimbunga Matthews Haki miliki ya picha AP
Image caption Jamaica pia imeathirika na kimbunga Matthews

Kimbunga Matthew kinaelekea kupita katika visiwa vya Caribbean - utabiri unaonyesha kitapita kati kati mwa magharibi mwa Haiti, ambako ndio kimeanza kutua, na mashariki mwa ukingo wa Cuba kinachotarajiwa kutua kufikia mwishoni mwa Jumanne.

Lakini kimbunga Matthew ni kikubwa, na kinasogea taratibu.

Katika maeneo mabako kinatarajiwa kupita, kutashuhudiwa upepo mkali wa kasi ya maili 140 kwa saa na mvua ya urefu wa hadi mita moja.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Haiti magahribi ndio itakayo athirika pakubwa
Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Sehemu kadhaa za kiiwa hicho zimeathirika tayari
Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Wakaazi wengi wanaishi katika makaazi duni kiabo kinasema 'Nyumba ya inauzwa'

Maeneo kadhaa ya pwani tayari yamefurika.

Lakini Haiti nzima imo hatarini ya kukumbwa na mchanganyiko wa mvua kali, mafuriko na saa kadhaa za upepo mkali.

Katika mji mkuu Port-au-Prince, mitaa miwili ya mabanda, La Saline na Cite Soleil, ambapo watu takriban nusu milioni wanaishi, ipo katika kima cha bahari.

Serikali imejaribu kuwashawishi wakaazi hao waondoke, lakini usafiri wa umma ni duni na watu wengi wanao hofia kuporwa na wamekataa kuondoka.