Serikali ya Colombia na FARC kupitia tena vipengele vya makubaliano ya amani

Rais wa Colombia, Juan Manuel Santos
Image caption Rais wa Colombia, Juan Manuel Santos

Serikali ya Colombia imeanza tena mazungumzo na kundi la waasi la FARC ili kujaribu kutafuta njia ya kufikia muafaka wa makubaliano ya amani baada ya matokeo ya kura ya maoni yaliyopatikana Jumapili iliyopita.

Pande hizo mbili zinakutana katika mji mkuu wa Cuba, Havana mara tu baada ya wananchi wa nchi hiyo kukataa vigezo vilivyokuwepo katika makubaliano hao.

Ingawa pande zote mbili zina nia ya kumaliza mapigano yaliyodumu kwa zaidi ya miongo mitano lakini rais wa zamani wa nchi hiyo Alvaro Uribe amekuwa akisisitiza majadiliano hayo kurudiwa. Hali inayomfanya rais Juan Manuel Santos kupanga kukutana na rais huyo wa zamani hii leo.

Wakati huo huo, tume ya serikali inatarajia kukutana na wajumbe waliopiga kura ya hapana ili kuweza kubaini vigezo ambavyo wangevikubali.