Jeshi la Syria kupunguza mashambulizi, Allepo

Gari lililoshambuliwa katika eneo la mashariki la Aleppo, Syria Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Gari lililoshambuliwa katika eneo la mashariki la Aleppo, Syria

Jeshi la Syria limesema litapunguza upigaji wake wa makombora katika eneo la Mashariki la Aleppo linaloshikiliwa na waasi, ambako mamia ya raia wameuawa wakiwemo watoto, katika kipindi cha wiki mbili zilizopita.

Katika taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari, jeshi hilo limesema limechukua uamuzi baada ya mafanikio yaliyoyapata katika operesheni zake ilizofanya Allepo.

Limesema upunguzaji huo wa mashambulizi ya anga na mizinga utaruhusu wakaazi wa maeneo hayo kwenda kuishi katika maeneo salama iwapo watataka.

Mashambulizi hayo ya hivi karibuni yaliyokuwa yakifanywa na serikali na kuungwa mkono na Urusi yameshutumiwa vikali.

Yalifanyika muda mfupi tu baada ya kuvunjika kwa makubaliano ya kusitisha mapigano.