Wana wa Kiume kurithi '' kasoro za uzazi za baba''

Wavulana waliozaliwa na baba wenye kasoro za uzazi hurithi kasoro hiyo Haki miliki ya picha Science Photo Library
Image caption Mbinu ya Kisayansi ya kutunga mimba

Wavulana waliozaliwa na baba ambao wana matatizo ya kutoweza kuwafanya wanawake kutunga mimba huenda wakawa na kasoro sawa na hivyo ikilinganishwa na wenzao waliotungwa kwa njiya ya kaiwaida.

Hii ni kwa mujibu wa utafiti mpya wa afya ya uzazi. Watafiti wamesema kwamba wavulana ambao baba zao hushindwa kuwafanya wanawake kutunga mimba watarithi matatizo hayo ya kizazi.

Wanasayansi hutumia njiya ya kutoa manii ya mwanamme aliye na uchache wake na kisha kuyadunga kwenye mayai ya mwanammke ili kutunga mimba. Mbinu hii ilianzishwa miaka ya tisini.

Watafiti walifawafanyia uchunguzi wanaume waliozaliwa kwa kwa njiya ya kutoa manii ya baba zao na kudunga kwenye mayai ya mwanammke na kugundua kwamba walikua na kasoro sawa na baba zao. Kwa mujibu wa mtafiti mkuu Profesa Andre Van Steirteghem amesema hii ndiyo mara ya kwanza imebainishwa kwamba watoto wa kiume wanaweza kurithi kasoro za uzazi zilizo na baba zao.