Uhaba wa walimu tatizo kubwa katika elimu Afrika
Huwezi kusikiliza tena

Uhaba wa walimu tatizo kubwa katika elimu Afrika

Wakati nchi zote duniani zinajitahidi kufikia malengo ya maendeleo endelevu ifikapo mwaka 2030, sekta ya elimu inatajwa kulegalega.

Changamoto kubwa ni ukosefu wa walimu ambako kuna wakati, madarasa yanalazimika kufungwa kwa kutokuwa na walimu wa kutosha.

Umoja wa Mataifa unazitaka serikali kuwekeza zaidi kwenye elimu na kuajiri walimu wengi zaidi. Iwe hatua ya dharura na lazima hasa kwa bara la Asia na Afrika Kusini mwa jangwa la Sahara ambako hali ni mbaya zaidi.

Mwandishi wetu Dayo Yusuf ametembela shule ya Olympic ambayo ni moja kati ya shule zilizoathirika zaidi nchini Kenya.