Kiongozi wa Renamo ashambuliwa mjini Maputo

Image caption Kiongozi wa Chama cha Renamo adai mmoja wa Viongozi wake wa juu amepigwa risasi

Kiongozi mkuu wa chama cha upinzani cha Renamo nchini Msumbiji amesema mmoja wa viongozi wa juu wa chama chake amepigwa risasi na kufa katika ufukwe wa mjini Maputo.

Jeremias Pondeca ndiye anayerdaiwa kuuawa na alikuw mjumbe wa kamati maalumu ya kujaribu kuondoa tofauti kati ya serikali na chama hicho.

Haijafahamika mara moja kuwa ni nani aliyemuua kiongozi huyo aliyekuwa akifanya mazoezi katika eneo hilo la ufukwe.

Kumekuwa na mapigano kati ya jeshi la serikali na Renamo tangu kuzuka kwa mvutano kufuatia miaka miwili iliyopita.

Pande hizi mbili zilizusha mapigano ya wenyewe kwa wenyewe kwa miaka 16 yaliyomalizika mwaka 1992.