Kenya yalaumiwa kwa kukiuka sheria za wakimbizi

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Wakimbizi wamepewa hadi Novemba kurudi makwao

Kenya inakiuka sheria za kimataifa kwa kuwalazimisha wakimbizi kwenye kubwa zaidi duniani kurudi nchini Somalia ifikapo mwezi Novemba, kwa mujibu wa shirika maarufu la utoaji misaada la Norwegian Refugee Council (NRC).

Utawala nchini Kenya ulihamrisha kufungwa kwa kambi ya Dadaab ambapo zaidi ya wakimbizi 280,000 kutoka nchini Somalia wanaishi.

Mkurugenzi mkuu wa shirika la NRC Jan Egeland anasma kuwa tarehe ya mwisho iliyotangazwa inastahili kufutwa kwa sababu imesababisa kutokea mvurugano kwenye shughuli ya kurejeshwa kwa wakimbizi.

Mwezi Agosti asilimia 74 ya wakimbizi wa Somalia walio kambi ya Dadaab walisema hawahisi kurudi Somalia wakiwa wanahofia usalama wao.

Neil Turner, ambaye ni mkurugenzi wa NRC nchini Kenya anasema mpango wa kurudi kwa wakimbizi haustahili kuwa wa kuwapeleka tena watu kwenye kambi nchini Somalia au kuwarejesha tena Kenya kama wakimbizi wasiosajiliwa.