Wito umetolewa kulinda 'mapafu ya bahari'

Zostera marina ni mmea ulipo kwa wingi kaskazini mwa dunia Haki miliki ya picha DAVID WROBEL, VISUALS UNLIMITED /SPL
Image caption Nyasi za baharini hupatikana katika maji madogo kwenye pwani

Zaidi ya wanasayansi 100 kutoka mataifa 28 wanataka hatua za kimataifa zichukuliwe kulinda nyasi za baharini.

Nyasi hizo hupatikani katika maji ya kupwa baharini.

Tofuati na gugu maji, nyasi hizo ni chakula na hifadhi kwa viumbe vya baharini na ndege.

Nyasi nyingi huharibiwa kwa shughuli za binaadamu, wanasema watafiti.

Katika taarifa, wanasayansi hao wanasema: "nyasi za baharini ni muhimu kwa samaki kutaga mayai na maeneo ya kuvuwa samaki duniani.

"Kupotea kwa nyasi hizo kunahatarisha kipato cha mamilioni ya watu na kinatoa nafasi kwa watu wengi kuingi katika kiwango kinachoongezeka cha umaskini.

"Pia inahatarisha uhai wa baadhi ya viumbe vya baharini kama kaa.

Dr Richard Unsworth wa chuo kikuu cha Swansea ndio anayeongoza kampeni ya kuokoa nyasi hizo.

'Mapafu ya bahari'

Taarifa ya muungano wa kuokoa nyasi hizo imechapishwa kufuatia kuwadia mkutano wa kimataifa kuhusu uhifadhi wake katika Wales kaskazini baadaye mwezi Ocktoba.

Nyasi za baharini hupatikana katika maji madogo kwenye pwani ya kila bara isipokuwa Antarctica, na zinapungua duniani kwa kiasi ya 2% kwa mwaka.

Nyasi hizo zinatambulika kama "mapafu ya bahari" kutokana na uwezo wake kuzalisha hewa safi ya oxygen.