Mutharika kurudi nyumbani Jumapili

Mutharika aliondoka nchini Malawi tarehe 15 mwezi Septemba
Image caption Mutharika aliondoka nchini Malawi tarehe 15 mwezi Septemba

Raia wa Malawi katika mtandao wa Twitter wamekuwa wakitumia hashtag #BringBackMutharika kujadilia alikoenda rais wao.

Rais Peter Mutharika alisafiri kuhudhuria mkutanoa wa Umoja wa Mataifa mjini New York tarehe 15 mwezi Septemba, na tangu wakati huo hajaonekana tangu atoe hotuba yake tarehe 21 mwezi Septemba.

Siku ya Jumatatu serikali ilitupilia mbali uvumi kuhusu afya yake baada ya kukosa kurejea kutoka nchini Marekani ikisema kuwa kuendelea kusambaza uvumi huo ni haramu.

Sasa serikali imetoa taarifa ikisema kuwa atarudi siku ya Jumapili ukiwa ni mweiz mmoja tangu aondoke.